“Ni kama tumeishia hapa kwenye jumba la kumbukumbu la kurekebisha uridhi wa ukoloni”

Mwanaharakati Mwazulu Diyabanza alipotembelea Antwerp: "Chifu Ne Kuko lazima arudi nyumbani!”

© Elien Spillebeen

Kwa mda wa miezi kadhaa zilizopita, mwanaharakati Mwazulu Diyabanza amejaribu, kuondoa sanaa za Kiafrika zilizoporwa kutoka Majumba ya kumbukumbu ya Uropa. Kwa ombi la MO *, alitembelea maonyesho ya Antwerp “100 x Kongo” kwenye Jumba la kumbukumbu la “De Stroom (MAS)”, ambapo alikutana na mratibu wa taswiri hadharani — Nadia Nsayi na jeshi ndogo la walinzi wa vyumba vya urithi wa umma.

Kwa mda wa miezi kadhaa zilizopita, mwanaharakati Mwazulu Diyabanza amejaribu, kuondoa sanaa za Kiafrika zilizoporwa kutoka Majumba ya kumbukumbu ya Uropa. Kwa ombi la MO *, alitembelea maonyesho ya Antwerp “100 x Kongo” kwenye Jumba la kumbukumbu la “De Stroom (MAS)”, ambapo alikutana na mratibu wa taswiri hadharani — Nadia Nsayi na jeshi ndogo la walinzi wa vyumba vya urithi wa umma.

Kuna yule atakaedhania kwamba, mwanaharakati wa Kongo Mwazulu Diyabanza Siwa Lemba ni kama “Robin Hood” ambaye anataka kurudisha urithi wa Kiafrika kule zilizo porwa. Kuna yule atakaedhania kwamba, yeye ni mwizi ambaye huiba vitu vya thamani kutoka kwa majumba vya kumbukumbu.

Mwezi Juni alijaribu kutoka kwenye jumba la kumbukumbu la “Quai Branly” huko Paris Ufaransa, na sanamu kutoka Chad. Katika jumba la kumbukumbu la Afrika huko Berg en Dal, Uholandi, alienda nje kupata hewa safi akibeba sanamu la kaburi kutoka enzi za ukoloni hadi alipokamatwa na polisi. Jumba la kumbukumbu la Afrika huko Tervuren pia alishalitembelea. Wiki hii ilikuwa zamu ya jumba la kumbukumbu la “De Stroom” (MAS) hapa Antwerp, ingawa wakati huu ziara yake lilitarajiwa.

Sio mwizi, ila ni mwanaharakati atakaye kurudisha sanaa ziliyoporwa kwa wamiliki halali. Hivyo ndivyo alivyojitambulisha kwa hakimu wa korti ya Ufaransa wiki iliyopita. Jumaa ijayo hakimu huyo atatoa uamuzi kuhusu kesi ya Quai Branly.

“Majumba za kumbukumbu zinamiliki urithi huu wa Kiafrika kwa kinyume cha sheria!” Daima anasisitiza ujumbe huu wakati wa vitendo vyake ambavyo vinaweza kufuatwa moja kwa moja mitandaoni kwenye social media. Maelfu ya wafadhili wanamtia moyo wakati wa ziara zake zenye utataa kwa vyumba vya kumbukumbu.

Tazama video ya ziara hiyo kwenye Facebook hapa chini:

Kwa mwaliko wa MO * alikuja kutoka Parisi huko Ufaransa kwenda Antwerp. Walinzi wa urithi wa MAS wamejiandaa kwa kuja kwake. Lakini mgeni naye kachelewa. Wafadhili watatu kutoka Liège walisafiri kwenda Antwerp spesheli kwa tukio hilo. Nadia Nsayi, mratibu wa taswiri hadharani na msimamizi mwenza wa maonyesho ya100 x Kongo — karne ya sanaa ya Kongo huko Antwerp, wanasubiri kuwasili kwa Mwazulu nao.

“Je! Mumepanga mwongozo wa MKongo haswa kwa ajili yetu?”

Wakati huo huo, Nsayi anawatambulisha kwa mwongozo mpya kabisa wa Antwerp-Kongo Marie-Antoinette Kumudidi Walo. “Je! Mumepanga mwongozo wa MKongo haswa kwa ajili yetu?” Anauliza Laety, mmoja wa wanaharakati kutoka Liège, kwa kinyuma. ‘Hapana sio hivyo. Tunayo miongozo mitano ya asili ya WaBelgo-Kongo kwa maonyesho haya. Miongozo ya Marie-Antoinette ziko katika lugha za Kilingala na Kifaransa. “Pamoja wanashangazwa na ukweli wa kwamba miongozo kutoka kwa diaspora ya Kiafrika hawapatikani kwenye maonyesho juu ya urithi wao.

Hapana, hawakujua kuwa Antwerp ina mkusanyiko mwingi hivyo wa vitu vilivyopatikana wakati wa ukoloni. “Mimi mwenyewe niliishi Antwerp kwa miaka mitatu na sikuijua pia”, anakubali Nsayi, “hadi nilipokuja kufanya kazi kwa MAS.”

Wamenaswa nyuma ya glasi

Akiwa na washiriki Wafaransa wa harakati yake ya Kiupan-Afrika Unité Dignité Courage, na akiwa na simu ya rununu tayari mkononi, kwa kichelewesho kidogo mwanaharakati huyo mwenye haiba mwishowe anaingia kwenye MAS.

Ukweli lisemwe, sio kila jumba la kumbukumbu litakubali kumfungulia milango yake mwanaharakati ambaye kawaida hatokani mkono mtupu. Lakini MAS haiogopi makabiliano kama haya. ” Tangu mwanzo Ilikuwa muhimu sana kwa jumba hili la kumbukumbu kwamba maonyesho haya yasiwe ya enzi zilizopita, ila ziwe pia za kuhusu enzi zijazo. Hatutaepuka kujiuliza uridhi wa Kiafrika zilizoporwa zafaa kuwa wapi.”

“Maonyesho haya sio tu ya zamani. Hatutaepuka kujiuliza uridhi wa Kiafrika zilizoporwa zafaa kuwa wapi”

Karne moja iliyopita, jiji la Antwerp lilianza kukusanya vitu vya urithi wa Wakongo. Hizi vitu haviwezi kutenganishwa na historia ya ukoloni. Karne moja baadaye, Els De Palmenaer na Nadia Nsayi sasa wamekusanya vitu mia moja ili kuziadharanishia uma.

De Palmenaer, mhifadhi wa Afrika ambaye amekuwa akisoma juu ja mkusanyiko huo wa uridhi wa Kiafrika kwa miaka mingi, alichukua fursa hiyo kumfanya mkaazi wa Antwerp, Nadia naye pia afikirie juu ya mkusanyiko huo. Kwa msaada wa watafiti Wakongo, wachunguzi hawa wana uwazi mkubwa iwezekanavyo kuhusu asili ya nyaraka hii. Watengenezaji filamu na wasanii wananoa historia ya kikoloni la mji wa Antwerp.

“Yeyote ataetembelea maonyesho haya anaweza kukosa utulivu. Kiini kwamba mkusanyiko huu haina ishara ya utulivu” anasema Nsayi, ambaye asili yake ya Kikongo ilimchochea kushiriki katika maonyesho haya.

Mwanzoni, kamera ya Mwazulu na mtiririko wa moja kwa moja ilisababisha hali ya wasiwasi. Je, aliitikia mwaliko huu kwa kusudi gani? Hilo ndilo swali ambalo linapepea hewani. Vipande havifai kuwa kwenye majumba ya kumbukumbu, aliteta waziwazi hapo awali. “Utajiri huu wa thamani kubwa yako gerezani leo hii.” Nyuma ya glasi kuna sanamu mbili za Kuba ambazo, kulingana na inavyosemekana, ni za karne ya 17 au 18. Wanaharakati waliopo wanatikisa vichwa kwa umakubaliano

“Kama unavyoona kuna walinzi wengi hapa”, mwanaharakati huyo anawaelezea wazi watazamaji wake moja kwa moja katika social media. Mwanzoni kuna watazamaji 500 na mwisho wa ziara yake, karibu watazamaji 10,000 wanafuata ziara hiyo mkondoni.

Walinzi wanajitahidi kadiri wawezavyo kukaa kimya, lakini ni vigumu kukana kuwa wako wengi zaidi ya kawaida. “Pia kuna madarasa ya shule hapa”, Nsayi anajaribu kutuliza hali. “Je! Glasi hii imewekwa haswa kwa sababu yangu?” Anamuuliza mara mbili.

© Elien Spillebeen

Sanaa ya ujambazi

“Tulikopa sanamu ya mpishi Ne Kuko kutoka Tervuren haswa kwa maaonyesho haya, kwa sababu ilionyeshwa hapa mnamo 1885 kwenye Maonyesho ya Dunia. Lakini pia kwa sababu ni fursa ya kuzungumza kuhusu sanamu hii ilivyopatikana, ambayo ilikuwa kwa njia ya vurugu sana.”

“Mara tatu tayari ombi la kurejeshwa kwa sanamu ya mpishi Ne Kuko, anayejulikana kama mfano wa sanamu zilizoporwa, imesha fanywa”

Nsayi anasema wazi wazi. “Tunajua kwa hakika kwamba iliibiwa na Mbelgiji.” Sanamu ya mpishi Ne Kuko inajulikana kimataifa kama mfano muhimu wa sanamu zilizoporwa au uporaji wa uridhi kisanii wa Kiafrika. “La hasha, hapa kuna mfano mwingine wazi wa sanamu iliyoporwa”, Nsayi anasema.

“Ne Kuko.” Mwazulu anairudia mara kadhaa, akiangalia sanamu hiyo moja kwa moja machoni. Licha ya ziara yake mapema huko Tervuren, anaonekana kuona sanamu hiyo kwa mara ya kwanza. Kwamba sanamu hiyo hapa inavutia sio kishangazo kwa Nsayi. “Hiyo ndiyo nia haswa.”

“Mwishoni mwa karne ya 19, chifu wa kijiji cha Kikuku alikuwa ameomba sanamu hii irejeshwe. Swali lake lilipuuzwa, “Nsayi anaelezea. “Rais Mobutu pia aliomba kurejeshwa kwa sanamu hii kipindi cha 1970. Hata mnamo 2016, chifu wa kisasa wa Kikuku alirudia ombi hilo.”

“Haya basi. Umeshuhudia hadithi hii yote”, anamsemesha sanamu hiyo ya nguvu ya kuvutia. Kisha anageukia wafuasi wake mkondoni: “Waziri wetu wa Utamaduni wa Ufaransa pia anasema kwamba swali hilo linapaswa kuulizwa rasmi.” Anamwonyesha Ne Kuko. “Hapa. Nitawaacha mufikirie wenyewe.” Kwa hatua kubwa anaendelea kupitia maonyesho.

Makumbusho ya Ukoloni

Marejesho, kurudisha vile vilivyohamishwa, haihusu vitu tuu, bali pia yahusu mabaki ya kimwili. Hii inadhihirika kwa kile kinachoonekana kuwa jalada kwa Wakongo waliokufa wakati wa Maonyesho ya Dunia mnamo 1894. Mgeni huyo anaona majina manane ya vijana wa Kongo ambao walilazimika kukaa kwenye hifadhi ya wanyama huko Antwerp, lakini kwa sababu ya hali mbaya hawakuponea utamasha hizo.

“Hapana, lazima warudi nyumbani.”

Uchunguzi wa jumba la kumbukumbu inaonyesha kwamba wafu hao watapatikana katika makaburi ya Schoonselhof. “Pamoja na baadhi ya wakaazi wa diaspora ya Kongo huko Antwerp, jiji linataka kutafakari jiwe la ukumbusho hivi karibuni.” Mwazulu anatikisa kichwa kukataa. “Hapana, lazima warudi nyumbani.”

© Elien Spillebeen

Kiti cha kifalme wa Tshokwe.

“Ningependa kuuliza tukae kimya hapa kwa dakika moja”, Nsayi anapendekeza. Ushuru kwa wahasiriwa hawa waliokufa bure, ila kwa burudani ya Magharibi, inaruhusu mapumziko kwa ziara hiyo ambayo tangu hapo awali ilikuwa bila utulivu. Kwenya maonyesho ya moja kwa moja ya Mwazulu kwenye social media, emoji za roho zinajaa.

Kile Mwazulu anafikiria kuhusu maonyesho haya kufikia katikati ya ziara hiyo bado ni ngumu kuamua. Mara kwa mara husimama kutoa maoni yake kwa watazamaji. Kwa mfano, anasema kuwa kiti cha kifalme cha Tshokwe sio lulu tuu ya kupendeza, ila pia kwamba kuiba kiti cha kiongozi au ufalme ulitimiza kusudi la kisiasa, ambayo ni ya kudhoofisha nguvu za ufalme.

Kwake mwongozo Marie-Antoinette, kiti hiki cha mfalme kina umuhimu mkuu katika mkusanyiko huu. “Sisi Wakongo tunaoishi Ubelgiji ni kama hadi leo bado haturuhusiwi kuketi. Hatupati upumziko hapa, hatuna utulivu. Usumbufu unabaki.”

© MAS

Picha ya Kuba ya kughushi chuma kutoka karne ya 17 au 18

Sanamu hizo mbili za Kuba, zilizoghushiwa kutoka kwa chuma, zinamhamasisha Mwazulu hadi kujizungumzisha mwenyewe ambapo anaanza kwa ukali: “Kuna sanamu tatu kama hizi ulimwenguni. Mbili ziko hapa. Jee Afrika? Ni lini watoto waliozaliwa Afrika watajua kwamba mkuu huyu, babu yao, alighushi sanamu hii? Ikiwa mungeweza kusikiliza kama mimi, mungesikia maumivu ya watoto Afrika. Maisha yao ya baadaye yaliibiwa na kuporwa.”

“Maelezo hayo tuliyopata mda mfupi uliopita, hatujawahi kuyasikia hapo awali kwenye jumba lolote la kumbukumbu.” Sauti ya Mwazulu inabadilika. “Ni kama kwamba tumeishia hapa kwenye jumba la kumbukumbu la kurekebisha uridhi wa ukoloni, ambapo watu wanazungumza juu ya asili na uhalifu.” Uwazi ambao maonyesho hayo yanataja majina na matendo hadharani, anasema, ni hatua muhimu ya kurekebisha yaliyopita.

Wafuasi kwenye Facebook ambao walikuwa wakimtarajia achukue kitu na kutafuta njia ya kutoka nacho nje wanaonekana ni kama leo hii matarajio yao hayatatimizwa.

Lakini Mwazulu anajua jinsi ya kujibu hisia na matarajio ya wasikilizaji wake. Ghafla anachukua kitambaa kilichopambwa cha raffia kutoka ukutani, akionekana wazi kuwa ana haki ya kitambaa hicho. “Ah, mheshimiwa …”, Nsayi anajibu, akiwatupia macho walinzi kwa kifupi, akitumaini hawatajibu kwa uharaka sana.

“Jee kitambaa hiki chanin’ginia hapa tangu linii? Unajiuliza. “Laa, toka juzi tuu” Kitambara hiki ni kazi yaka msanii Bren Heymans na wapamba rafia kutoka Kasaï. Mwazulu anarejesha kitambaa hicho na kuendelea hadi kwa kabati uliofungwa. “Waelewa kwamba yote haya ni mali yetu? Kabati hizi zafunguliwa vipi ili kukarabatishwa?”

© Elien Spillebeen

Décoloniser wa déradicaliser

“Je! Unaitazamaje Kongo ya sasa?” Swali hili ndilo maonyesho haya yanaishia. “Je, hatima ya mkusanyiko huu ni ipi? Tiyari tunajua kwamba Mwazulu ana jibu”, Nsayi pia anajua. Lakini watunzaji na walinzi wa urithi wa MAS wanataka kila mgeni atafakari juu ya swali hili.

Katika kitabu “Binti wa Ukoloni”, kilichochapishwa hivi karibuni na Nadia Nsayi. Nadia anaandika kwamba hajioni kama mhifadhi, ila kama mtetezi wa kikomesho cha itikadi ya kikoloni. Je, Mwazulu anafikiria kuwa Nsayi amefaulu katika hichi kitetezo kupitia maonyesho ya 100 x Kongo?

“Wanaharakati wanahitaji habari na maarifa ili wafaulu na shinikizo zao za kisiasa”

“Ikiwa anajiita mtetezi wa kikomesho cha itikadi ya kikoloni, basi ninaiheshimu uamuzi wa vile anavyojitambulisha”, anasema kidiplomasia tunapokaa kando baada ya ziara. Maonyesho ya moja kwa moja ya ziara hii unasimamishwa na wanaharakati wengine wanachukua mapumziko kiasi. “Anaelezea hadharani hadithi sahihi ya mkusanyiko huu na hilo ni jambo la ubunifu.” Ingawa Mwazulu angependa kuona Nsayi akichukua hatua inayofuata: ” Ombi la kurudishiwa kwa urithi huu. Inapaswa kuuliza kila mgeni kusaidia kuhakikisha kuwa vitu hivi vitarudishwa nyumbani.”

“Hilo ni jukumu la mwanaharakati”, anajibu Nsayi. “Kazi yangu ni kuhabarisha na kuwezesha mjadala. Uamuzi juu ya ukombozi uko mikononi mwa jiji la Antwerp. Lakini ili kuchukua hatua za kisiasa, kuweka shinikizo la kisiasa, wanaharakati wanahitaji habari na maarifa. Ninaamini kwamba utakapoondoka kwenye jumba hili la kumbukumbu pia utakuwa umepata habari mpya.”

Ingawaje njia zao zinatofautiana, Nsayi na Mwazulu wanakubaliana kwa mafikirio kadhaa. Kwa mfano, wote wawili wana matarajio makubwa ya diaspora ya Kiafrika huko Uropa. Nsayi: “Maonyesho haya yanaisha Machi. Lakini sijui tutajipata wapi kijamii baada ya miezi sita. Kamati ya bunge imeanza hivi karibuni, ambayo itazingatia hali ya ukombozi wa wakoloni na marudisho ya sanamu zilizoporwa. Jamii za wabelgiji, na sana sana zile za diaspora za Kiafrika zinazoishi hapa, zinaweza kuchukua jukumu muhimu na kuamua kuendelea na mijadala zao. Lakini itabidi tuone kama hizi jamii za diaspora zinauwezo wa kujipanga na kujichangia vyema ili zifaulu kujisongesha mbele.”

Nsayi anasema anapenda kushiriki na vijana wa diaspora za Kiafrika na ughaibuni: “Historia inatufundisha kwamba hizo sio haki ambazo watu wanakupatia bila hivyo hivyo. Hizo sio zawadi. Lazima zilazimishwe. “Mwazulu anakubali”, Sheria yeyote inayomaliza udhalimu, kama ile ya utumwa, ilitanguliwa na vita.”

ⓒ Elien Spillebeen

Nsayi na Mwazulu wanatumaini kwamba kitambulisho cha kizazi kinategemea mabara mawili kwa sababu Ulaya umeweka mpira katika upande wa Afrika. Viongozi wa nchi za Ulaya na majumba ya kumbukumbu wanasubiri swali rasmi kutoka kwa viongozi wa nchi za Afrika. Lakini viongozi wa Kiafrika, kama vile Rais wa Kongo Félix Tshisekedi, wameamua wazi wazi kwamba urejesho wa sanamu sio kipaumbele kwa sasa.

“Ikiwa diaspora za Kiafrika zingependelea maendeleo, inabidi zijiepuke kwa adhari kuhusiana nchi zao asili ingawaje kipaumbele hakiko huko sasa, kwa sababu hizo siasa za Kiafrika ziko kawaida kabisa. WaAfrika wana wasiwasi tofauti za uhai kila siku, “Nsayi anaelewa. “Kwa hivyo watu kutoka ughaibuni lazima wachukue jukumu muhimu lililopangwa.” Kulingana na Nadia, “Ukosefu wa utamaduni na kitambulisho, ni shida kubwa ambacho kinabidi nchi kama Kongo ikubaliane kindani na serikali za Ulaya hata bila kuelewa siasa zao za ukoloni binafsi.

Hakuna chochote kitatokea leo ikiwa hautasikilizika!” Mwazulu anaonya. Anatambua kuwa vitendo vyake kwenye majumba ya kumbukumbu ni muhimu sana na inaweka wazi kuwa haifai kujitokeleza bila vurugu. “Ikiwa hatusikilizi upinzani wa amani sasa”, anaongeza Nsayi, “itabidi upinzani wa ukali utumiwe. Ikiwa jamii haizungumzi kwa umakini juu ya ubaguzi wa rangi na haki ya watu wote, tujajipata kwa msimamo mkali unaoweza kusababisha ukosekano wa utulivu kati ya jamii zetu.

Kurudi nyumbani

Katika kitabu chake, Nsayi pia anapendekeza kwamba tunaweza kuhitaji ugeuzaji wa meza kihalali. Sasa nchi yetu, au katika kesi hii, jiji la Antwerp, ndiye mwamiliki wa hati. Serikali ya Ubelgiji inaweza kuamua kwamba hati hizo zihamishwe kihalali au zikopeshwe kwa Kongo. Kama mwandishi, Nsayi anawasilisha wazo la kurejesha sanamu zilizoporwa kwa majumba ya kumbukumbu ya Kongo. Isitoshe, Kongo inasubiri sanamu za babu zao zirudishwe ili wamiliki wa kisasa waziweke kwa mkopo.

Kwa matendo yake, Mwazulu anafanya ionekane kwamba analaani haki za mali halali na anaamini kwamba anaweza kuondoka na urithi wa Kiafrika. Hata hivyo haoni ukweli halisi wa kisheria. Anaangalia pia jinsi vitendo vya Unité Dignité Ujasiri vinaweza pia kupanuliwa kisheria. “Tuko tayari kupinga haki za mali. Kwa sababu unaweza kumpiga Mike Tyson barabarani, lakini hiyo haijalishi ikiwa hauwezi kumpiga kulingana na sheria za pete.”

Mwazulu anasisitiza kwamba sheria yenyewe haina haki. “Ikiwa nitachukua kifaa chako cha kurekodi hapa sasa na kisha nitie hati ambayo inasema kuwa ni yangu na kisha nikakuuliza uthibitishe kinyume, hiyo ni udhalimu gani?”

“Ni sasa tu nimekumbuka: nilikuja hapa leo kumrudisha Ne Kuko nyumbani!”

Mwazulu hakubali kwamba ni maafisa rasmi wa Kiafrika tu ambao wanaweza kuuliza hati hizo. Yeye humchukulia mpishi wa jadi au jamaa aliyebaki, au kama msemaji, kama alivyoidhinishwa kurudisha kitu kilichoibiwa.

Ikiwa angeondoka na sanamu hiyo kutoka kwa Berg en Dal — au kipande chochote baadaye — angempa nani? “Kumtolea mkuu wa nchi inaonekana kama mtihani wa kuvutia kwangu, ili tu kuona jinsi wanavyoshughulikia hiyo sanaa.” Lakini mwishowe haamini kwamba kurudi kunapaswa kupitia njia hiyo ikiwa wataishia kwenye jumba la kumbukumbu la Afrika. “Hizo hati lazima ziende kwa idadi ya watu, watu ambao ni wenyewe.”

“Ninaona wazo hilo kuwa la kuvutia. Nilitembelea majumba mapya ya kumbukumbu huko Kinshasa mwaka uliopita. Ingawaje ni bure, ni watu wachache sana waKongo wanaoweza kwenda huko. “Nsayi pia anaona ni ubaba sana kwamba nchi za Magharibi zingeweka masharti ya ukombozi na kuamua njia ya uhifadhi.

Sanamu yenye nguvu, iliyoibiwa kutoka kwa mikono ya chifu Ne Kuko, inachukuliwa kama mfano. Kipande hicho kimejadiliwa mara kadhaa katika mazungumzo tofauti. “Sasa najua!” Mwazulu anasema kwa ghafla. “Ni sasa tu ninakumbuka kwamba nilikuja hapa leo kumrudisha Ne Kuko nyumbani!”

“Lazima tuende ghorofani baadaye. Tunapaswa kumchukua Ne Kuko pamoja nasi,”, Mwazulu anamwambia mwenzake ambaye kwa kweli alitaka kusema kwamba kituo cha vijana cha mkondoni AJ + kinasubiri mahojiano na Mwazulu. “Ndio, sawa. Lakini Chifu Ne Kuko anahitaji kurudishwa nyumbani haraka!”

© Elien Spillebeen

Maonyesho 100 x Kongo — karne ya sanaa za Kongo huko Antwerp kwenye Jumba la kumbukumbu la “De Stroom” (MAS) huko Antwerp itaendelea hadi mwisho wa Machi 2021.

Maak MO* mee mogelijk.

Word proMO* net als 2938   andere lezers en maak MO* mee mogelijk. Zo blijven al onze verhalen gratis online beschikbaar voor iédereen.

Ik word proMO*    Ik doe liever een gift

Over de auteur